WIKI YA KUWASILIANA NA MBINGU

| Makala

WIKI YA MAWASILIANO NA MBINGU: 

February 19 - February 25,2024

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo lihimidiwe, Shalom Shalom,

Madhabahuni tupo kwenye ratiba maalum ya maombi ya mfungo wa siku 7 za kuwasiliana na KITI CHA ENZI mbinguni kwa habari ya maisha yetu ya kila siku.

Mungu wakati wote amekuwa akiahidi mambo mengi sana yenye baraka kwa maisha yetu, lakini ahadi hizo haziwezi kujileta au kutokea kienyeji bila kutengeneza mahusiano yetu na mtoa ahadi aliyetuahidi.

Suala la kutoa ahadi kutoka kwa Mungu ni jambo moja, kupokea ahadi ni jambo lingine ambalo linahusisha kuwekeza kiroho kwa baadhi ya maeneo haya muhimu sana; 

#AHADI ZA MUNGU KUTIMIA KWAKO, ZINAAMBATANA NA KANUNI UNAZOTAKIWA ANAZOKUPA MUNGU NA KUZIFUATA KWA MAKINI

1} Kuwa msomaji wa Neno la Mungu, maana kwa njia hii ndipo utazijua zaidi ahadi za Mungu kwako

2} Kuwa mtu wa kutafakari sana Neno la Mungu unalolisoma kila wakati, usisome biblia kama hadithi au gazeti, yatafakari maneno unayoyasoma

3} Kuwa na ratiba sahihi na ya kueleweka kwa kuwekeza muda wa kutosha kwenye maombi, Na haya ni maombi ya kumkumbusha Bwana Mungu kwa kile alichokiahidi kwako kuwa atakutendea, kile ulichokisoma kwenye Biblia na ukakitafakari, Simama na hicho kwa kumkumbusha Mungu, Biblia inasema Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.

Pastor Innocent Mashauri

Madhabahu ya siri za biblia

Maarifa ya ki-Mungu

+255 758 708 804


 SADAKA